Sunday, May 11, 2025
Home Soka TPLB Yamjibu Kocha Azam Fc

TPLB Yamjibu Kocha Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Bodi ya ligi kuu Tanzani imetolea ufafanuzi ombi la kocha mkuu wa klabu ya Azam fc Aristica Cioaba aliyeomba kuongezwa idadi ya wachezaji wa kufanyia mabadiliko kutoka watatu mpaka watano.

Kocha huyo alitoa ombi hilo ili kuepusha wachezaji kupata majeraha kutokana na kutocheza kwa muda muda mrefu baada ya ligi kuu kusimamishwa kupisha janga la ugonjwa wa corona huku wakitakiwa kucheza mechi mfululizo endapo ligi itarejea.

Akijibu kuhusu ombi hilo mtendaji mkuu wa bodi hiyo Almas Kasongo alisema ni ngumu kubadili kanuni hasa katikati ya msimu lakini watalichukua na kulifanyia kazi ikiwezekana.

banner

Mimi nafikiri tulichukue ili wakati wa uboreshaji wa kanuni zetu tuliwasilishe lakini sioni kama kuna hiyo nafasi katikati ya msimu. Kwahiyo tutakapotangaza maboresho ya kanuni ni vizuri tukalichukua hilo“, amesema Kasongo.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.