Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Ufukweni imefuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya ushindi wa jumla wa mabao 12-9 dhidi ya Burundi katika michezo yote iliyochezwa katika fukwe za Coco Dar es salaam.
Licha ya leo Tanzania kufungwa mabao 6-4 katika mchezo wa marudiano lakini ushindi wa mabao 8-3 katika mchezo wa kwanza umewabeba Tanzania.