Connect with us

Soka

Simba yataja Afisa habari mpya

Klabu ya soka ya Simba imemtangaza mtangazaji wa michezo wa Azam media Ahmed Ally kuwa Afisa habari na mawasiliano mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Ezekiel Kamwaga aliyekuwa akikaimu baada ya kuondoka kwa Haji Manara.

Mwanahabari huyo mwenye uzoefu wa kutosha katika tasnia hiyo,amefanya kazi kwa muda mrefu kwenye vituo vya Sahara media kupitia startv kabla ya kuelekea Azam tv baada ya kujizolea umaarufu mkubwa kwa wadau wa michezo mbalimbali hapa Tanzania.

Ahmed ameshafanya kazi na Simba katika matukio na hafla mbalimbali za klabu hiyo kama vile hafla za utoaji wa tuzo kwa wachezaji waliofanya vizuri,na anajulikana kwa jinsi anavyoipamba timu hiyo kila anapokuwa kwenye majukumu yake ya kikazi katika kituo chake cha Azam tv.

Hata hivyo wadau mbalimbali wa soka nchini wanasubiri kuona ni kitu gani ataenda kuifanyia klabu hiyo kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na watangulizi wake kipindi cha nyuma,lakini hakuna shaka juu ya taaluma wake na uwezo wa kushughulika na maswala ya aina hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka