1
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Taifa Stars Mbwana Samatta ‘Poppa’ na washambuliaji Simon Msuva na Yohana Mkomola wanatarajiwa kuwasili kwenye kambi ya timu hiyo mapema Leo.
Taarifa kutoka Jijini Nairobi, Kenya ilipo kambi ya Stars zinaeleza kuwa nyota hao watatu watawasiri mapema kesho nchini humo tayari kwa kuungana na wenzao ambao wapo hapo kambini tangu Machi 13 mwaka huu.
Nyota hao walichelewa kufika kambini hapo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya klabu zao, Samatta Akiwa Fenerbahce ya Uturuki, Msuva akiwa Wydad Casablanca ya Morocco na Mkomola akiwa Ingulets Petrove ya Ukraine.