Connect with us

Soka

Manara Amjibu Msemaji Azam Fc

Mkuu wa kitengo cha habari ndani ya klabu ya Simba sc Haji Manara amemjibu Msemaji wa klabu ya Azam Fc Zaka Zakazi ambaye alisema klabu ya Simba sc imetwaa ubingwa kwa kubebwa na marefa wa ligi kuu nchini.

Zakazi alitoa kauli hiyo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari nchini kuhusu ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara.

Kufuatia kauli hiyo ya Msemaji huyo wa klabu ya Azam fc,Manara nae hakuwa nyuma baada ya kujibu kauli hiyo ya Zakazi.

“Nimesikia msemaji wao kasema maneno ya ovyo ubingwa wetu wakupewa sisi tunaheshimu” Manara

“Msemaji wa Azam fc anasema ubingwa wetu wa kununua anashindwa kutuheshimu tunapoint 79 wao 58 unafungwa na Kagera sugar unadroo biashara tunakufunga nje ndani tena hauna mchezaji mwenye goli 9 sisi tunamchezaji ana magoli 19 unasemaje sisi ubingwa wetu wa ovyo”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka