Friday, May 9, 2025
Home Soka Man Utd Yakomaa na Sancho

Man Utd Yakomaa na Sancho

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester united inaamini itaipiku Chelsea kwenye mbio za kuwania saini ya Kiungo mshambuliaji na winga Jodan Sancho anayechezea klabu ya Dortmund ya Ujerumani.

Jordan Sancho anadaiwa kuwa na thamani ya Pauni milion 120 ambapo klabu yake ya Dortmund ipo tayari kumuuza kwa timu itakayofikia thamani hiyo kwa mchezaji waliyemnunua kwa Paundi milioni 8 kutoka Manchester city.

United haina budi kukabiliana na Chelsea katika mbio za kumuwania winga huyo ambaye inaonekana angependelea zaidi kurudi nyumbani huku kocha Frank Lampard akiwa na ubavu wa kushindina na United baada ya kuwa hela za kutosha baada ya kutosajili kwa madirisha mawili yaliyopita.

banner

Manchester United wanapewa kipaumbele kumsajili mchezaji huyo aliyeweka rekodi ya kufunga mabao 25 kabla ya kufikisha umri miaka 20 katika ligi ya bundesliga baada ya kumuandalia malipo mazuri huku Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Ed Woordward akiahidi uwekezaji wa kutosha katika kikosi hicho.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.