Mshambuliaji wa klabu ya Horoya ya Guinea Mkongomani Heritier Makambo amefikia makubaliano kuvunja mkataba na timu kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Makambo alijiunga na Horoya 2019 akitokea kwa wananchi Yanga Afrika alikocheza kwa mafanikio makubwa kwa kufunga mabao 18 ya ligi kuu ya Vodacom kabla ya kuondoka.
Hatua hiyo inahusishwa na mshambuliaji huyo kutakiwa tena na waajiri wake wa zamani ambao wamekuwa wakihaha kupata mrithi wake tangu aondoke bila mafanikio,licha ya kusajiri washambulia kadhaa kama Juma Balinya,David Molinga,Yikpe,Sarpong,Waziri Junior na Nchimbi.