Connect with us

Soka

Kocha Madrid Ajiunga Sevilla

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya hispania na klabu ya Real Madrid  Julen Lopetegui ameteuliwa kuwa meneja wa timu ya Sevilla kwa mkataba wa miaka mitatu kuanzia jana.

Lopetegui 52,Alikua kocha wa timu ya taifa hilo wakati wa fainali za kombe la dunia 2018 na alitimuliwa siku mbili kabla ya michuano hiyo kuanza baada kujulikana kuwa baada ya fainali hizo ataenda kujiunga na Real Madrid.Sababu kubwa ya kutimuliwa kwa kocha hiyo katika kambi ya timu ya taifa hilo ni kuepusha kuwagawa wachezaji wa timu ya taifa kambini hapo kutokana na uhasama uliokuwepo baina ya klabu za madrid na barcelona za nchini humo.

Kocha huyo baadaye alifukuzwa na Real Madrid baada ya kuifundisha kwa takribani miezi minne baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha uwanjani hasa baada ya kupata kipigo cha 5-1 kutoka kwa mahasimu wao Barcelona.

Sevilla ambao walitembelea nchini wiki chache zilizopita,walimaliza ligi hiyo ya Laliga katika nafasi ya sita huku wakimtimua meneja wao Paulo Manchin baada ya matokeo mabaya katika michuano ya ulaya(Ueropa league).

Sevilla iliyoanzishwa mwaka 1890 inatumia uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan kama uwanja wake wa nyumbani wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 54,883 waliokaa.Uliitwa jina hilo kama kumbukumbu ya Rais wa zamani wa klabu hiyo Ramon Sanchez Pizjuan aliyeiongoza kwa miaka 17 na ndiye muasisi wa ujenzi wa uwanja huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka