Iko hivi mastaa wawili wa klabu ya Yanga Mybin Kalengo na Issa Bigirimana wamerejea nchini kwao kwenda kujiuguza majereaha waliyoyapata wakati wakiitumikia timu hiyo hapa nchini.
Kalengo amerejea nchini Zambia baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu alioumia wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba mkoani Mwanza huku Bigirimana anaendelea na matibabu ya nyama za paja ambazo zinamsumbia kwa muda mrefu.
Mastaa hao wote wameshindwa kuitumika timu hiyo kwa muda mrefu baada ya kusumbuliwa na majeraha na hivyo kuweka rehani nafasi zao kikosini humo.