Inasemekana Uongozi wa kipa wa Simba , Beno Kakolanya umefikia pazuri kwenye mazungumzo Juu ya kumpeleka kipa huyo katika timu mpya kwa msimu ujao baada ya kukosa namba katika klabu ya Simba sc.
Beno ametokea kuvivutia vilabu viwili huku ikifahamika kimoja ni cha ndani ya nchi huku klabu nyingine ikitajwa kuwa ni ya nje nchi japo haijafahamika wazi ni nchi gani.
Mazungumzo kwa vilabu vyote yanaenda vizuri na mwishoni mwa msimu huu uongozi wake utaamua aende wapi kucheza soka huku pia habari za ndani zikidai kuwa mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya ndani ya Simba sc yamesimama kwasasa.