Kocha mkuu wa kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba sc Mfaransa Didier Gomes ameitahadharisha klabu ya Yanga kujiandaa vizuri kwani wao Simba wamejipanga kulipiza kisasi kwenye mchezo huo wa fainali wa kombe la shirikisho.
Gomes ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo wa fainali utakaopigwa mkoani Kigoma tarehe 25 mwezi Julai.
Alisema”matokeo ya mchezo wa Julai 3 yalituumiza sana sisi na mashabiki zetu hivyo tumejipanga kulipa kisasi,tumerekebisha makosa tuliyofanya katika mchezo uliopita na tumeongezea baaadhi ya vitu kwani malengo yetu ni kushinda ubingwa huo”.
Simba na Yanga zitakutana kwa mara kwanza katika fainali za michuano hiyo tangu ianze, na mchezo huo utapigwa katika dimba la Lake Tanganyika mwisho wa reli Kigoma.