Chelsea na Liverpool wamedondosha alama mbili muhimu kila mmoja wikiendi hii kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza na kuiacha man city ikiongoza gepu la uongozi katika vita ya kuwania taji la ligi hiyo msimu wa 2021/2022 baada ya ushindi dhidi ya Newcastle.
Man city waliokuwa wa kwanza kucheza walipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Newcastle united walio katika hali mbaya.Magoli ya Ruben Diaz,Joao Cancelo,Riyad Mahrez na Raheem Sterling yalitosha kwa vijana hao wa Pep Guardiola kuondoka na alama zote tatu muhimu.
Chelsea waliosafiri hadi Moleneux kucheza na Wolvehampton walilazimishwa sare ya pili mfululuzo baada ya kutoka 0-0 dhidi ya mbwa mwitu hao.Matajiri hao wa London wameshindwa kupunguza gepu kati yake na vinara city zaidi ya kuongezeka na kufikia pointi sita.
Liverpool wao walikuwa London kuwakabili Tottenham Hotspurs ya Antonio Conte walilazimishwa pia sare ya 2-2 na kuwafanya city kwenda Christmas wakiwa kileleni kwa alama tatu zaidi yao.
Ligi hiyo itaendelea tena boxing day kwa michezo tisa baada ya bodi ya ligi hiyo kukataaa ombi la kusimamishwa kwa michezo kipindi hiki cha Christmas ili kukabiliana na ongezeko la Uviko-19.
Â