Wednesday, May 7, 2025
Home Soka Chelsea yadondosha alama,Liverpool yaikaba  koo City epl

Chelsea yadondosha alama,Liverpool yaikaba  koo City epl

by Sports Leo
0 comments

Vita ya kuwania taji la ligi kuu soka nchini Uingereza imeendelea usiku wa kuamkia leo ambapo Chelsea alishuka dimbani darajani  kuikabilisha Everton,huku Liverpool nao wakiwa nyumbani waliwakaribisha Newcastle United kwenye dimba la Anfield.

Chelsea wamedondosha alama mbili muhimu kwenye vita hiyo baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Everton huku wapinzani hao wakiwakosa mastaa wake kwenye kikosi cha kwanza kama Richarlison,Gray,Digne,Allan na Calvet Lewin.

Licha ya kuwakosa Lukaku,Timo Werner na Hudsoi Odoi bado Chelsea walikuwa na uwezo wa kuifunga Everton,lakini matumizi mabaya ya nafasi za kufunga yamewafanya kuzidi kutengeneza gepu kati yake na vinara Man City.

banner

Liverpool hawakufanya makosa kwa kupata ushindi mzuri wa 3-1 dhidi ya Newcastle United kupitia kwa Diogo Jota,Mohamed Salah na Trent Anold. Ushindi huo umewafanya waendelee kuongeza presha kwa City kileleni huku tofauti ikiwa ni alama moja tu.

Msimamo wa ligi hiyo baada ya michezo ya katikati ya wiki hii.

 

 

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.