Connect with us

Makala

Azam Fc Wazindua Rasmi Jezi za 2024/2025

Klabu ya Azam Fc imezindua rasmi jezi zake za msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa mapema hii leo katika boti ya Azam Marine wakielekea Visiwani Zanzibar huku wakishuhudiwa na maelfu ya mashabiki kupitia Azam Tv.

Jezi hizo za aina tatu za nyumbani,Ugenini na jezi ya tatu zimezinduliwa mchana wa leo zikiwa na rangi nyeupe,Blue na Nyeusi huku zote zikiwa zimechanganywa na rangi ya dhahabu mbele ya Mh.Tabia Mwita ambaye ni Waziri wa michezo Visiwani Zanzibar.

Mpaka sasa tayari jezi hizo zinapatikana katika maduka mbalimbali Zanzibar na ndani ya jiji la Dar es salaam.

Msimu huu Azam Fc sambamba na kumaliza wa pili katika ligi kuu nchini pia watashiriki michuano ya kimataifa baada ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika na wanatarajiwa kuanza na Apr ya Rwanda katika hatua ya awali.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala