Home Masumbwi Mgunda Aondoka Simba sc

Mgunda Aondoka Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa klabu ya Simba sc Juma Mgunda ameondoka klabuni hapo kwa ruhusa maalumu na kuamua kurejea nyumbani kwao jijini Tanga kutokana na matatizo binafsi ya kifamilia siku moja baada ya kocha mkuu wa klabu hiyo Roberto Oliveira “Robertinho” kurejea akitokea nyumbani kwao nchini Brazil.

Kuondoka kwa Mgunda kumepishana siku moja na kocha mkuu ambaye amerejea na kuchukua jukumu la kufanya maandalizi ya mwisho mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Singida Big Stars siku ya kesho utakaofanyika jijini Dar es salaam ambapo Robertinho na msaidizi wake watashika timu bila Mgunda kwa mara ya kwanza tangu wachukue jukumu la kuinoa timu hiyo.

Simba sc itakabiliwa na upinzani mkali katika mchezo huo dhidi ya Singida Big Stars ambapo vikosi vya timu zote mbili vimefanya sajili za maana zikiwa na mastaa mbalimbali wenye makali ya kutosha kuonyesha burudani kwa wananchi na mashabiki mbalimbali.

banner

Kila timu ina umuhimu wa kuchukua alama tatu katika mchezo huo baada ya awali kugawana alama katika mchezo wa duru ya kwanza katika uwanja wa Liti mjini Singida huku mpaka sasa Simba sc ina alama 50 nafasi ya pili na Singida Big Stars ikiwa na alama 43 nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited