Timu ya Yanga sc imeandika barua kwa shirikisho la soka nchini (Tff) kuomba kusogezwa mbele kwa mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Ruvu shooting ili kupata muda wa kupumzika kufuatia mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Township Rollers.
Kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo Said Khimji alisema timu hiyo inabanwa na ratiba kufuatia kusafiri jana kupitia Afrika kusini na baada ya mchezo huo utakaofanyika tarehe 24 na safari ya kurudi inatarajiwa kuwa tarehe 26 huku ikifika nchini tarehe 27 na kwa mujibu wa ratiba inatakiwa wacheze tarehe 28 siku moja baada ya kurudi nchini hivyo timu itakua haijapumzika hivyo akiomba mchezo kufanyika tarehe 30 mwezi huu.
Yanga imesafiri na kikosi cha wachezaji 20 ikiwaacha mastaa wapya Mustapha Selemani,David Moringa na Farouk Shikalo kufuatia kutopata leseni ya kushiriki michuano hiyo kutoka shirikisho la soka barani Afrika (Caf).