Klabu ya Yanga sc imelitingisha jiji la Dodoma baada ya kutua asubuhi ya leo na moja kwa moja kuelekea bungeni ambapo walikaribishwa kwa shangwe na wabunge mashabiki wa klabu hiyo.
Yanga sc ambao ni mabingwa mara 27 wa ligi kuu Tanzania bara wameingia jijini Dodoma kuelekea mchezo wa kesho wa ligi kuu dhidi ya Jkt Tanzania ambapo baada ya mchezo huo wataelekea mjini Shinyanga kuwavaa Mwadui Fc katika mchezo wa kombe la Fa.