Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amekiri timu hiyo kudaiwa na wanaendelea kulipa madeni hayo ambayo mengi wameyarithi kutoka katika uongozi uliopita.
Jana kuliibuka taarifa kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhisi wa Michezo (CAS) imeiamuru klabu ya Yanga kumlipa dola 20,000 aliyekuwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe ikiwa ni madai ya fedha za usajili na malimbikizo ya mishahara ya miezi mitatu
Mwakalebela amesema uongozi wao ulirithi madeni kutoka uongozi uliopita hivyo wanaendelea kuyalipa madeni hayo
“Tumerithi vitu vingi yakiwemo madeni kutoka kwa uongozi uliopita, hata hili deni ya Tambwe ni miongoni mwa madeni hayo. Tunawahakikishia Wanayanga kuwa deni hili litalipwa,” alisema Mwakalebela
Aidha Mwakalebela aliongeza kuwa pia watalipia fedha walizotakiwa walipe ili kesi yao dhidi Bernard Morrison iweze kusikilizwa na CAS