Klabu ya Yanga sc imelalamika kutotendewa haki na waamuzi wa ligi kuu nchini kiasi cha kusababisha kuwa na matukio mengi tata katika michezo inayowahusisha wao nchini.
Yanga sc kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari Hassan Bumbuli na Haji Manara wamefanya mkutano na waandishi wa habari kulalamika kuhusu uonevu huo ikiwemo kunyimwa nafasi za kufunga kwa kisingizio cha Offside pamoja na kupunjwa dakika za nyongeza baada ya dakika tisini za mchezo.
“Kumekuwa na mlolongo wa matukio ya maamuzi yenye utata ambayo kwa namna moja au nyingine yananyima haki ya timu zingine na yanatoa manufaa Kwa timu zingine,”Tunataka Waamuzi wetu waanze kujitafakari juu ya haya ambayo yamekuwa yakiendelea na yamekuwa mjadala mkubwa sana kwenye Taifa letu, Lakini pia tunataja mamlaka zinazosimamia mpira zichukue hatua juu ya jambo hili ambalo watu wamewekeza pesa zao”Alisema Bumbuli.