Imezoeleka kwa vilabu vya hapa nchini, havisajili wachezaji wenye mikataba, mara nyingi husubiri mikataba ifike mwisho kisha kusajili wachezaji walio huru
Hata hivyo Yanga kupitia wadhamini/wahisani wao GSM, usajili wa kuelekea msimu ujao watafanya mambo tofauti
Imeelezwa GSM walimpa mkufunzi wa Yanga Luc Eymael uhuru wa kupendekeza wachezaji anaotaka wasajiliwe bila ya kujali kama mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu au la
Mabilionea hao wamejipanga kutumia ‘fedhwa’ kufanya usajili wa maana na pengine kwa mara ya kwanza kwenye usajili ujao wa Yanga inaweza kushuhudiwa mchezaji akanunuliwa hata kwa Tsh Milioni 500 au zaidi ili mradi tu awe na sifa na pia awe amehitajika na kocha
Na ndio maana pamoja na kufahamu mshambuliaji Heritier Makambo kuwa na mkataba Horoya AC, klabu ya Yanga imeanza mazungumzo na klabu hiyo ili kuipa sahihi ya nyota huyo aliyejitengenezea jina licha ya kuitumikia Yanga kwa msimu mmoja tu
Jana Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alisema kampuni hiyo itashirikiana na uongozi wa Yanga kufanya usajili kabambe ambao wana uhakika utawapa ubingwa msimu ujao