Nahodha wa Tanzania,Mbwana Samatta amefanikiwa kujiunga na klabu ya Fenerbahce ya uturuki kwa mkataba wa miaka minne akitokea Aston Villa inayoshiriki ligi kuu England.
Samatta ameondoka Villa kutokana na nafasi yake ya uchezaji kuwa ndogo baada ya wachezaji wengine kusajiliwa na Aston Villa katika nafasi ya ushambuliaji wakiwemo Watkins na Traore.
Fenerbahce wamempatia jezi namba 12 nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania(Taifastars) ambaye anaenda kuongeza nguvu katika kikosi hicho kwani walikuwa wakimuwania mara kadhaa kabla ya kwenda Aston Villa.