3
Kamati ya maadili ya shirikisho la soka nchini (TFF) imemfungia miaka (5) kujihusisha na soka makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga sc Fredrick Lugano Lameck Mwakalebela.
Mkuu wa wilaya mstaafu, kiongozi wa zamani wa Mtibwa sugar na katibu mkuu wa zamani wa (TFF) Fredrick Mwakalebela amefungiwa kwa madai kuwa alitoa taarifa za uongo kwa kuituhumu (TFF) kuwa inaionea klabu ya Young Africans.
Â
Kwa mujibu wa Tff adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 73(4) cha kanuni ya maadili za Tff toleo la 2013.Barua Rasmi iliyotolewa na Tff hii hapa: