Kwa mujibu wa Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc Barbara Gonzalez kiungo mpya wa klabu hiyo Thadeo Lwanga anasumbuliwa na majeraha ndio maana hajaonekana uwanjani mpaka sasa.
Usajili wa mchezaji huyo umeleta sintofahamu kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na mchezaji huyo kushindwa kuonekana uwanjani licha ya taratibu za usajili kukamilika ambapo tetesi zilizagaa kuwa hajapata hati ya kimataifa ya uhamisho(Itc).
Majibu ya Barbara yamehitimisha mjadala kuhusu kiungo huyo ambaye wengi walidhani atacheza mchezo wa kimataifa siku ya jumatano dhidi ya Fc Platnum kutokana na kukosekana kwa Jonas Mkude aliyesimamishwa.