Wednesday, May 14, 2025
Home Makala Liverpool On Top Na Pointi 70

Liverpool On Top Na Pointi 70

by Sports Leo
0 comments

Liverpool imebaki nafasi ya kwanza ikiwa imewapiga West Ham United mabao 2-0 katika michuano ya ligi kuu England siku ya jana uwanja wa London Stadium wakisimamiwa na refa kutoka England Jonathan Moss.

Mshambuliaji wa liverpool Mohamed Salah alianza kuipatia bao la kwanza timu yake kupitia penalti aliyopewa na Jonathan ikiwa ni adhabu ya Westham dakika ya 35 huku bao la pili lilipatikana dakika ya 52 kupitia Alex Oxlade Chamberlain.

Wachezaji wawili wa WestHam ndio waliopokea kadi za njano katika mchezo wa jana ambao ni Issa Diop dakika ya 34 na dakika ya 43 alipokea Mark Noble.

banner

West Ham United inabaki kushika mkia nafasi ya 17  na pointi 23 ikiwa imecheza mechi 24 huku Liverpool inabaki nafasi ya 1 ikiwa imecheza mechi 24 na pointi 70 zenye kuleta furaha kwa mashabiki wake.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.