Uongozi wa klabu ya Namungo Fc umemuondoa kikosini mwao golikipa Beno Kakolanya kutokana na matukio ya utovu wa nidhamu ambayo amekuwa akiyafanya mara kwa mara.
Kakolanya ameondolewa kikosini humo alipokuwa akitumika kwa mkopo akitokea klabu ya Singida Black Stars na sasa atarejea katika klabu yake mkoani Singida.
Kipa huyo mkongwe ambaye amezichezea klabu za Simba sc na Yanga sc kwa nyakati tofauti amekua na matatizo ya kinidhamu mara kwa mara tangu akiwa katika klabu hizo.
Mpaka sasa haijafahamika msimamo rasmi wa klabu yake ya Singida Black Stars kuhusu suala hilo kama itampokea ama lah.
Kakolanya katika ubora wake alikua ni kipa mwenye uwezo mkubwa hasa wa kucheza mipira ya uso kwa uso na washambuliaji hatari nchini kiasi cha kupata nafasi katika kikosi cha timu ya Taifa nchini.