Kusimamishwa kwa mashindano ya soka nchini kwa muda wa mwezi mmoja imekuwa fursa kwa wachezaji wa timu mbalimbali kupumzisha mwili na kujiweka fiti kabla ya kuendelea na soka siku zijazo.
Serikali ilisimamisha mashindano hayo na utekelezaji wake ukafanywa na shirikisho la mpira wa miguu (TFF) ikiwa ni miongoni mwa hatua za kujikinga na virusi vya Corona.
Baada ya wachezaji kucheza idadi kubwa ya mechi kwa muda wa miezi mitatu mfululizo bila kupata mapumziko,hii inakuwa fursa kwao kupumzika na familia zao huku wakijikinga na virusi vya Corona vilivyoingia nchini 15,machi 2020 kupitia mwanamama Isabella.