Saturday, May 10, 2025
Home Makala Azam Tv,Tff Zaingia Mkataba

Azam Tv,Tff Zaingia Mkataba

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la soka nchini Tanzania limesaini mkataba wa miaka minne na kampuni ya Azam Media kwa ajili ya kuonesha moja kwa moja mechi za Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mkataba huo wa kuonesha mechi za Taifa Stars umegharimu shilingi milioni 400 ambazo ni sawa shilingi milioni 100 kwa mwaka kwa muda wa miaka minne, na kwenye kila mechi Taifa Stars itapata shilingi milioni 35 kutoka Azam Media.

Wakipeana mikono baada ya kusaini mikataba hiyo.

Mkataba wa awali wa Azam Sports umefikia tamati msimu uliopita na sasa pande hizo zimesaini mkataba mpya wa miaka minne wenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 mbele ya waandishi wa habari huku Tff ikiwakilishwa na Rais Warrace Karia na Katibu mkuu Wilfred Kidao huku Tido Mhando na Patrick Kahemele wakiwakilisha upande wa Azam Media.

banner

Akitoa ufafanuzi wa mkataba huo Mkuruguenzi wa Michezo wa Azam Media Patrick Kahemele amesema mechi za Taifa Stars zilizodhamini na Azam ni zile za kirafiki zitakazokuwa kwenye kalenda ya FIFA.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.