Beki wa kushoto wa Atletico Madrid ya Hispania ambaye ni raia wa Brazil,Renan Lodi amethibitika kukutwa na virusi vya Corona.
Lodi alianza kuonesha dalili za kuwa na virusi vya Corona mwanzoni mwa Machi lakini hakuwa amechukuliwa vipimo hadi wiki hii alipopimwa na kuthibitika kukutwa na virusi hivyo.
Hata hivyo wachezaji 9 wengine wa klabu hiyo ya Atletico Madrid wamepimwa na kukuta hawana maambukizi hivyo kuruhusiwa kuanza mazoezi.