Friday, May 9, 2025
Home Soka ‘Mnisamehe’-Ronaldo De Lima

‘Mnisamehe’-Ronaldo De Lima

by Sports Leo
0 comments

Gwiji wa soka wa Brazil Ronaldo Delima ameomba radhi kwa wamama wote duniani ambao watoto wao walivutiwa na kuiga mtindo wake wa kunyoa nywele nusu wakati wa fainali za kombe la dunia mwaka 2002.
.
bapo Ronaldo pia amesema kuwa alifanya hivyo kuondoa mitizamo ya mashabiki kuhusu utimamu wake wa mwili baada ya kupata majeraha kabla ya kuiongoza Brazil katika ubingwa kwenye michuano hiyo ya dunia mwaka huo.

Katika fainali za kombe la dunia mwaka 2002 Ronaldo alimaliza akiwa ni mfungaji bora kwa kufunga mabao 8 huku akitwaa kiatu cha dhahabu.

Katika mchezo wa fainali wa mechi hizo zilizofanyika Korea na Japan Brazil walitwaa kombe la dunia kwa kuwafunga Ujerumani mabao 2-0 ambapo katika mchezo huo Ronaldo aliingia uwanjani akiwa amenyoa mtindo huo ambao baadae watoto wengi duniani walitamani kunyoa kama yeye huku wengine wakigombana na wazazi wao.

banner

Ronaldo amenukuliwa akisema kuwa “Ninaomba radhi sana kwa wamama wote ambao watoto wao walinyoa kama hivyo”.
Huku akiendelea kusema kuwa “Waandishi wa habari walisahau kuhusu majeraha yangu baada ya mtindo huo wa nywele na niliwauliza kuwa mmeupenda? lakini wao walisema hapana mbaya zinyoe”. Alisema Ronaldo Delima.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.