Tuesday, May 13, 2025
Home Soka Kocha Mbabe Wa Zahera Atimuliwa

Kocha Mbabe Wa Zahera Atimuliwa

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco imemfuta kazi kocha wake Mkuu Sebastian Desabre mwezi mmoja tu tangu imteue kushika nafasi hiyo.

Tukio hilo limekuja baada ya Wydad kupoteza mchezo wake wa ligi wikiendi hii  na klabu ya Difaa El-Jadid kwa Bao pekee la Winga Simon Msuva na baada ya mechi hiyo Desabre amefukuzwa baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha.

Desabre ndiye aliyeiongoza Pyramids Fc kuwafunga Yanga iliyokua chini ya Mwnyi Zahera nyumbani na ugenini katika michuano ya kombe la shirikisho na kuhitimisha safari ya kocha Mwinyi Zahera katika michuano ya kimataifa akiwa Yanga.

banner

Kocha huyo ni kama amekuwa na mkosi kwa sasa kwani anafukuzwa mara ya pili ndani ya msimu huu, hii ni baada ya kufukuzwa na Pyrmids Fc ambayo licha ya kufanya vzuri katika kombe ka shrikisho barani Afrika, kiu yao kubwa ilikuwa pia katika ligi ya nchini Misri.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.