Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazingisa amewateua Rispa Hatibu kuwa kuwa msaidizi wake huku pia akimteua kuwa mkurugenzi wa wanachama na mashabiki uteuzi ambao umeanza rasmi leo novemba mosi.
Senzo alikua hana msaidizi tangu alipoteuliwa na klabu hiyo mwezi septemba akitokea nchin Afrika kusini alipokua akifanya kazi mbalimbali za michezo hasa katika klabu za soka nchini humo kama Orland pirates na Platnum stars.
Taarifa kutoka klabuni hapo imeonyesha kuwakaribisha wakurugenzi hao wapya.