Connect with us

Soka

Sterling Asababisha Rais Kujiuzulu

Rais w shirikisho la soka la Bulgaria Borislav Mihaylov amejiuzulu nafasi hiyo kufuatia vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyoonyesha na mashabiki pamoja na wachezaji wa taifa hilo katika mchezo dhidi ya England kuwania nafasi ya kufuzu michuano ya mataifa ya ulaya mwaka 2020.

mashabiki waliokua wakitoa ishara za kibaguzi uwanjani hapo.

Mchezo huo ambao ulifanyika katika mji wa Safia nchini humo uliisha kwa England kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 mabao ya marcus rashford,Raheem sterling(2),Delle Ali(2) na Harry Kane ambapo mchezo ulilazimika kusimama mara mbili kufuatia ubaguzi huo kwa wachezaji weusi wa England akiwemo Raheem Sterling.

Rais huyo amejiuzulu kufuatia shinikizo la waziri mkuu wa nchi hiyo aliyemtaka rais huyo kujiuzulu kufuatia tukio hilo lisilokubalika katika michezo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka