Connect with us

Soka

Yondani Arejea Kishingo Upande

Beki kisiki wa Yanga sc Kelvin Yondani amerejea klabuni hapo na kujiunga na kambi ya mazoezi ya klabu hiyo huku akisisitiza kumaliziwa stahiki zake zote anazoidai klabu hiyo.

Inasemekana beki huyo alikubali kuzungumza na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo na kufikia makubaliano ya kumaliza tofauti hizo huku akiahidiwa kuwa madai yake yatashughulikiwa huku akiwa kambini na timu hiyo kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ugenini nchini Botswana.

Yondani na wenzake Juma Abdul na Andrew Vicent wanadaiwa kugoma ili kushinikiza uongozi kuwalipa madai yao ya fedha za usajili wanazodai baada ya klabu hiyo kusajili wachezaji wapya na kuwalipa fedha zao zote ilihali wao wakiendelea kusubiri tangu fedha za mwaka jana.

Awali kocha Mwinyi Zahera alisisitiza beki huyo ana ruhusa maalumu hivyo atajiunga na timu hiyo hivi karibuni huku akiweka bayana kuhusu mgomo wa Juma Abdul na Andrew Vicent kuwa wana madai ya msingi hivyo wanapaswa kusikilizwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka