Yanga,Gwambina Yahamishiwa Uhuru

0

Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha mabadiliko ya uwanja utakaotumika leo kwenye mchezo wa raundi ya tano kombe la FA dhidi ya Gwambina Fc.

Mchezo huo umehamishiwa uwanja wa Uhuru kutoka uwanja wa Taifa ambao ulipangwa awali huku Mabadiliko hayo yametokana na uwanja wa Taifa kufungwa kwa ajili ya matengenezo madogo madogo.

Mchezo huo utapigwa saa kumi Alasiri badala ya saa  moja usiku iliyotangazwa awali huku mshindi atafuzu hatua ya robo fainali.

Leave A Reply

Your email address will not be published.