Yanga Yawasili Bukoba

0

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kufika salama mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar utakaofanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Kaitaba mkoani humo.

Yanga imewasili ikiwa na kikosi chote cha mastaa iliyowasajili msimu huu wakiwemo Michael Sarpong,Carlos Carlinhos,Yacouba Signe,Tuisila Kisinda pamoja na Mukoko Tonombe huku ikiwa na lengo la kutwaa pointi tatu dhidi ya walima miwa hao waliochini ya kocha Mecky Mexime.

Yanga tayari imevuna alama nne kati ya sita huku Kagera Sugar ikivuna alama moja kati ya sita baada ya timu zote kucheza mechi mbili.

Leave A Reply

Your email address will not be published.