Yanga Waituliza Mbeya City

0

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuifunga klabu ya Mbeya City Fc bao 1-0 mchezo wa ligi kuu uliochezwa usiku huu katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Matokeo ya michezo iliyopita kwa timu zote mbili yalisababisha presha kubwa katika mchezo huo ambapo Yanga sc walihitaji kujiweka katika nafasi sahihi baada ya kusuluhu mechi ya kwanza dhidi ya Prisons huku Mbeya city wakipokea kipigo kutoka kwa Prisons.

Lamine Moro ndie shujaa kwa upande wa Yanga baada ya kufunga goli hilo akiunganisha kona ya Carlos Carlinhos dakika ya 87 bao lililoduma mpaka mwisho mwa mchezo.

Yanga wamepanda mpaka nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 4 huku Kmc wakiwa kileleni mwa msimamo na Mbeya city wakiwa mkiani baada ya kupoteza mechi zote mbili.

Leave A Reply

Your email address will not be published.