Connect with us

Soka

Yanga Wachana Mbao Taifa

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbao katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ulifanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mabingwa hao wa kihistoria walifanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 18 likifungwa na David Molinga kwa penati baada ya Feisal Salum kuangushwa ndani ya eneo la mita 18 ambapo kipa Rahim Abdalah alishindwa kuipangua.

Licha ya kosa kosa za hapa na Pale Yanga ilishindwa kupata bao la pili hadi dakika ya 81 ambapo pasi ya Tariq Seif Kiakala ilirukwa na Mrisho Ngasa na kumkuta Patrick Sibomana aliyefunga bao la pili na kukamilisha ushindi huo.

Yanga bado inashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo japo ikiwa na mechi mbili mkononi na jumapili itakutana na watani wa jadi Simba sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka