Connect with us

Makala

Yanga sc Yachukua Alama Tatu Mbeya

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Kengold Fc uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Ikianza na mastaa wake wakiongozwa na Cletous Chama na Stephan Aziz Ki huku wakisaidiwa na Clement Mzize,Duke Abuya na Khalid Aucho huku eneo la ulinzi likiwa na Yao Kouasi Attouhoula,Dickson Job,Ibrahim Hamad Bacca na Chadrack Boka huku golini akisimama kipa Djigui Diarra.

Krosi iliyotokana na faulo iliyopigwa na Azizi Ki ilimkuta Ibrahim Hamad Bacca na kufunga kwa kichwa bao la pekee katika mchezo huo dakika ya 13 ya mchezo huo huku kipindi cha kwanza kikiisha kwa Yanga sc kukosa nafasi kadhaa za wazi.

Licha ya mabadiliko ya mwalimu Gamondi kuwaingiza Dube na Pacome Zouzoua bado Yanga sc haikuweza kupata bao lolote huku Kengold Fc nusra wapate bao dakika za mwishoni mwa mchezo.

Kocha Miguel Gamondi alisema kuwa kikosi chake hakikua na mchezo mzuri lakini anafurahia alama tatu muhimu walizopata.

“Nina furaha na matokeo maana alama tatu ni muhimu sana kwetu, tulikosa nafasi za wazi nyingi kipindi cha kwanza”.Alisema Miguel Gamondi kocha mkuu wa Yanga sc.

Kutokana na ushindi huo sasa Yanga sc imefikisha alama sita huku ikiwa imecheza michezo miwili na Kengold ikiwa mkiani mwa msimamo bila alama huku ikiwa imecheza michezo mitano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala