Home Soka Yanga sc Vs Geita Gold Sc Shirikisho

Yanga sc Vs Geita Gold Sc Shirikisho

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc itakutana na Geita Gold sc katika mchezo wa robo fainali ya kombe la shirikisho la AzamSports kutokana na droo iliyofanyika mapema hivi leo katika ofisi za Azamtv jijini Dar es salaam.

Jumla ya timu nane zimeshiriki droo hiyo mbele ya wawakilishi wa vilabu hiyo ambapo Yanga sc itamenyana na Geita Gold sc ambao wametoka kucheza nao siku ya jumapili jioni na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu nchini na endapo watafuzu watakutana na mshindi katika ya Singida Big Stars dhidi ya Mbeya City Fc.

Mechi hiyo inatarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam ambapo Yanga sc ni mwenyeji wa mchezo huo ambao kwa sasa klabu hiyo inatumia uwanja wa Azam Complex kama uwanja wa nyumbani baada ya uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa katika matengenezo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited