Connect with us

Soka

Yacouba Bado Bado

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Yacouba Sogne ataendelea kutoonekana uwanjani baada ya kutokupona majeraha yake yanayomsumbua kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Awali nyota huyo alikosa mechi za mwisho michuano ya kombe la mapinduzi ikiwemo mechi ya fainali dhidi ya Simba sc ameshindwa kupona baada ya kupatiwa matibabu ya awali na sasa italazimika arudishwe hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi ili kujua tatizo linalomsumbua.

Yacouba amekua na wakati mzuri katika mechi za ligi kuu kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita akifunga mara nne na kusaidia upatikanaji wa mabao matatu licha ya kutoanza msimu vizuri.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka