Connect with us

Soka

Tutashiriki Uefa-Guardiola

Man city Waajiri mwanasheria,kumlipa milioni 59 kwa siku kuhakikisha wanashinda rufaa ili kushiriki Uefa msimu ujao.

Man City imemuajiri mwanasheria maalumu ambaye atakuwa analipwa hela za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 59 KWA SIKU ( paundi elfu 20 ) ili aweze kuinasua timu ktk adhabu ya Kukosa Uefa kwa misimu wawili.

David Pannick ni jina la nguli huyo wa sheria wa viwango vya juu kutoka Uingereza ambaye ana jukumu hilo la kuhakikisha City inaondokana na adhabu hiyo baada ya kutajwa kuvunja sheria za matumizi ya fedha katika usajili.

Pannick ndiye aliyezuia mara mbili nchi ya Uingereza isijitoe ktk umoja wa Ulaya kwa kutofuata taratibu.

Pep Guardiola alikaririwa mwisho wa wiki hii akisema anaamini timu yake itashiriki Uefa msimu ujao na hili linaleta tumaini jipya kwao.

Cc:Priscakishamba

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka