Connect with us

Soka

Tetesi za Usajili Barani Ulaya

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann atajiunga na barcelona msimu ujao baada Mtendaji mkuu wa club ya Atletico Madrid kuthibitisha kuwa suala hilo lilishafikiwa muafaka tangu machi mwaka huu na kumaliza tetesi za muda mrefu kuhusu mstakabali wa mshambualiaji huyo aliyekuwa pia akihusishwa na man utd na Psg.Barcelona watalipa paundi 108m zilizoko katika mkataba wake.(skysports news)

Baada ya kutengewa Paundi 500m za usajili,Zinedine Zidane anahitaji kukamilisha usajili wa kiungo Paul Pogba haraka iwezekanavyo huku man utd ikidaiwa wako tayari kumuuza kwa dau la paundi 150m.Real madrid iko tayari kutoa paundi 100m kumnasa kiungo huyo anayetakiwa pia na juventus.

Middlesbrough watamtangaza Jonathan Woodgate kuwa meneja wao mpya baada ya kuondoka kwa Tonny Pullis,Woodgate alikua msaidizi wa msicotland huyo mpaka alipoondoka klabuni hapo.Inatajwa Robby Keane anahitajika kuungana na Woodgate kama kocha klabuni hapo.

Ferlan Mendy amekamilisha usajili wa kujiunga na Real Madrid akitokea Lyon baada ya kusaini mkataba wa miaka sita kwa dau la paundi 31m.Atatambulishwa wiki ijayo.

Tottenham wameanza mazungumzo na Lyon juu ya usajili wa kiungo Tanguy Ndombele japo mazungumzo hayo yapo katika hatua za awali,Juventusi pia wanatajwa kumuwania kiungo huyo mwenye miaka 22.

Man utd wameongeza juhudi kumuwania kiungo wa Sporting Lisbon Bruno Fernandez huku ikisemekana utd wamewazidi man city katika mbio hizo baada ya dau la paundi 70m kuonekana kuwashawishi mabosi wa timu hiyo,Kiungo huyo mwenye miaka 24 amefunga magoli 32 na kusaidia upatikanaji wa magoli 18 katika mechi 53 msimu uliopita.

Man utd wamesitisha mpango wa kumsajili Ghareth Bale iwe kwa jumla ama kwa mkopo licha ya kumtafuta kwa misimu kadhaa,inadaiwa madrid ipo tayari kumuachia mchezaji huyo ili kupata nafasi ya kusajili zaidi,Bale 29 analipwa paundi 350000 kwa wiki bernabeu.

Tetesi hizi ni kwa mujibu wa magazeti na mitandao mbalimbali duniani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka