Connect with us

Soka

Takukuru Yachunguza Mamilioni Tff

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) yawasiliana na CAF kuchunguza ushiriki wa rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia katika kashfa ya ubadhirifu wa fedha za CAF baada ya FIFA kumfungia rais wa CAF Ahmad Ahmad kutojihusisha na masuala ya soka kwa miaka 5 kutokana na kashfa ya ubadhirifu.

Inadaiwa Wallace Karia ni miongoni mwa wanufaika kwa kupata mgao wa dola 20,000 kutoka Caf ambazo zilikua kwa ajili ya matumizi ya Rais wa Shirikisho kwa mujibu wa Caf.

Akijibu kuhusu suala hilo Brig. Jen. John Mbungo,Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru alisema”Tumewasiliana na CAF, tumeanza uchunguzi, unajua hili suala ni jipya na ndio kwanza tumeanza uchunguzi, siwezi kuahidi itachukua muda gani, lazima kila hatua izingatiwe kwenye uchunguzi huu ili kama Wallace Karia amehusika na wote walionufaika na ubadhirifu huo waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Soka