Connect with us

Soka

Stars Yapigwa na Bulgaria

Timu ya Taifa ya Tanzania  ‘Taifa Stars’ imeanza vibaya mechi za kirafiki za kalenda ya Fifa ‘Fifa series’ baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Bulgaria katika mchezo uliofanyika katika mji wa Baku nchini Azerbaijan jioni ya machi 22.

Licha ya kupoteza mchezo huo Taifa Stars inabidi ijilaume yenyewe kutokana na kupoteza nafasi bora ya kutangulia kufunga dakika ya 28 kupitia nafasi ya wazi ya winga wa klabu ya Simba sc  Kibu Denis ambaye shuti lake liligonga  mwamba na kumkuta tena Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye alipaisha mpira huo wa “Rebound”.

Stars ilipata pigo baada ya kipa Aishi Manula kuumia dakika ya 30 na kutolewa uwanjani baada ya kupata maumivu na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na Kwesi Kawawa aliyekwenda kumalizia dakika 60 za mchezo huo.

Bao hilo lililoamua mchezo huo lilipatikana dakika ya 51 kwa njia ya mpira wa adhabu ndogo likifungwa na kiungo na nahodha wa Bulgaria, Kiril Despodov ambapo kipa Kawawa pamoja na jitihada zote alishindwa kuokoa shuti hilo.

Haikuwa siku nzuri kwa Fei Toto kwenye mchezo huo baada ya kupoteza nafasi nyingine ya wazi katika dakika ya 72 akiunasa mpira uliotokana na kujichanganya kwa mabeki wa Bulgaria, lakini shuti lake akiwa uso kwa usok na kipa wa wapinzani akapaisha.

Matokeo hayo yanaifanya Stars kubakiza mchezo mmoja wa mwisho dhidi ya Mongolia utakaopigwa Machi 25 ambao utakamilisha ratiba ya mechi za kirafiki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka