Connect with us

Soka

Soksi Zawaponza Gwambina

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Septemba 15, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatao;

Mmassi: Gwambina FC ready to fight with the best in Tanzania league |  Goal.com

Mechi namba 2: Biashara United FC 1-0 Gwambina FC

Timu ya Gwambina FC imepewa onyo kali kwa kosa la kufika katika kikao cha kitaalamu cha maandalizi ya mchezo wakiwa na vifaa pungufu (kutokuwa na soksi kwa wachezaji wa ndani na walinda mlango).

Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 15:2 (2.2)-15(54) kuhusu taratibu za mchezo. Pia Gwambina FC imeonywa kwa kosa la kufika uwanjani wakiwa na vifaa pungufu kwa maana hawakuwa na soksi za wachezaji wa ndani wala walinda mlango hivyo kupelekea mchezo huo kuchelewa kuanza kwa takribani dakika 14 mpaka pale soksi zilipoletwa.

Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 15:(2.3):2.3.1)(2:3:2)(2.3.3)(2.3.4)(2.3.5)(2.3.6)(2.3.7) na 15:2(2.4)- 15(54) kuhusu taratibu za mchezo.

Uongozi wa timu ya Biashara United FC umekumbushwa kusimamia na kutimiza vema majukumu yake baada ya tukio la waokota mipira wao (ball kids) kuonekana kuchelewesha kwa makusudi kurusha mipira wakati wa
mchezo huo pia kupunguza idadi ya mipira mara tu baada ya timu hiyo kupata bao mnamo dakika ya 88 katika mchezo tajwa hapo juu uliochezwa Septemba 6, 2020 katika uwanja wa Karume (Musoma).

Pia Kamati imeutaka uongozi wa timu ya Biashara United ueleze kwanini waokota mipira wake (ball kids) walificha mipira na kuchelewa kurusha mipira uwanjani mara tu baada ya kupata bao dakika ya 88. Wachezaji Salum Kipaga wa Gwambina FC na Hamadi Waziri Tajiri wa Biashara United kila mmoja amesimamishwa kucheza mechi tatu
zinazofuata sambamba na kupigwa faini ya shilingi laki tano (500,000/=) kwa kosa la kupigana katika mchezo wa Biashara FC dhidi ya Gwambina FC.

Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 39:2(2.6) Udhibiti kwa wachezaji

Mechi namba 3: Dodoma FC 1-0 Mwadui FC

Uongozi wa timu ya Dodoma FC umekumbushwa kutimiza vema majukumu yake baada ya meneja wa uwanja wao wa nyumbani (Jamhuri Stadium), Antony Nyembelah kuonyesha tabia isiyo ya kiungwana ya kutokabidhi funguo za chumba cha kubadilishia nguo kwa timu ya Mwadui katika mchezo wao dhidi Mwadui FC uliochezwa Septemba 6, 2020 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Pia uongozi wa timu hiyo umekumbushwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo baada ya Meneja wa uwanja wao wa nyumbani pamoja na maafisa wa ulinzi wa uwanja huo kuruhusu magari na pikipiki kuingia uwanjani
wakati wa mchezo.

Mchezo namba 14: Mtibwa Sugar FC 1-1 Simba SC

Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar FC kupitia kwa meneja wa uwanja wao wa nyumbani wa Jamhuri, Morogoro umekumbushwa kutimiza majukumu yao ipasavyo baada ya kutenda makosa yafuatayo:

1. Kuruhusu magari kuingia ndani ya uwanja wakati mchezo ukiendelea.

2. Kuruhusu kuwekwa kwa bendera za chama cha siasa kwenyemilingoti usawa wa katikati ya uwanja hali inayokinzana na taratibu za mchezo. Pia milingoti hiyo inazuia wapiga picha na warusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu (Azam TV) kufanya kazi yao kwa uhuru huku wageni waliokaa jukwaa kuu wakishindwa kutazama mechi kwa ukamilifu wake.

Ahsante.
Idara ya Habari na Mawasiliano
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Septemba 17, 2020

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka