Connect with us

Soka

Simba sc Yaifuata Singida Big Stars

Klabu ya Simba sc imepaa kwa ndege kwenda mkoani Dodoma kisha kuunganisha kwenda Singida kwa gari kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars utakaofanyika siku ya Jumatano katika uwanja wa Liti mkoani Singida.

Hii ni mara ya kwanza timu hizo kukutana tangu Singida Big Stars ipande kucheza ligi kuu nchini msimu huu ambapo inatarajiwa kuwa mechi yenye ushindani mkubwa kwa klabu hizo kutokana na vikosi vya kusheheni mastaa wenye majina ikiwemo wale kutoka nje ya nchi kama Brazil,Senegal,Zambia na Malawi.

Simba sc ipo nafasi ya pili ya  msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama 17 huku ikiwa imecheza michezo 8 wakati Singida Big Stars ikiwa nafasi ya nne ya msimamo ikiwa na alama sawa na Simba sc japo yenyewe imecheza michezo tisa.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na mvuto zaidi endapo mastaa Meddie Kagere na Said Ndemla watacheza dhidi ya timu yao ya zamani ya Simba sc walioitumikia kwa miaka mingi zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Soka