Connect with us

Soka

Simba Sc Waituliza Kagera Sugar

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kupunguza pengo la alama kati yake na Vinara wa ligi kuu nchini Yanga sc baada ya jana kuifunga klabu ya Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

John Bocco alifanikiwa kufunga kwa penati dakika ya 42 baada ya Hassan Dilunga kuangushwa katika eneo la 18 na David Luhende na mpaka timu zinaingia mapumziko matokeo yalibaki hivyo hivyo.

Dakika ya 48 kipindi cha pili dakika ya 48 Said Ndemla aliipatia Simba sc bao la pili baada ya kufanya shambulizi la ghafla ambapo Cletous Chama alimpasia mfungaji ambaye aliukwamisha mpira nyavuni.

Simba sc sasa imepanda mpaka nafasi ya tatu ikiwa na alama 19 huku Yanga akiwa kinara kwa alama 23 ambapo timu hizo zitakutana siku ya jumamosi Novemba 7 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka