Connect with us

Makala

Simba Sc Kurudi kwa Fei Toto

Kwa mujibu wa taarifa za ndani Klabu ya Simba Sc itatuma rasmi maombi ya kumuhitaji Kiungo wa klabu ya Azam Fc Feisal Salum ili kukiongezea nguvu kikosi hicho hasa katika michuano ya Kimataifa.

Simba Sports Club inamuhitaji kuanzia dirisha dogo lakini pia itakuwa tayari kusubiri hadi dirisha kubwa kama itashindikana kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari.

Feisal amebakisha mkataba wa miaka miwili ya kusalia Azam Fc baada ya kumsajili kwa mkataba wa miaka mitatu msimu uliopita akitokea Yanga sc.

Azam Fc na Yanga sc waliweka vipengele vya kuitaarifu Yanga sc endapo watakua na mpango wa kumuuza staa ndani ya nchi huku pia wakiweka dau la dola laki 5 kwa timu inayotaka kumnunua staa huyo.

Simba sc itakutana na upinzani mkubwa kutoka Yanga sc ambao nao wanamhitaji staa huyo arejee klabuni hapo ikiwa ni miaka mmoja tangu aondoke kwa usajili ambao ulileta mtafuruku kiasi cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Samia Suluhu Hassan kuingilia kati.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala