Connect with us

Soka

Simba Sc Inanuka Pesa

Klabu ya Simba sc leo imesaini mkataba mnono wa miaka 2 na kampuni ya Romario Uhl Sports kwa ajili ya kutengeneza na kuuza jezi za klabu hiyo hapa nchini.

Mkataba huo wa miaka miwili umesainiwa hii leo baina ya Afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Crescentious Magori na mwakalishi wa Uhl hapa nchini Minhaal Dewji ambapo kampuni hiyo pia itatoa vifaa kwa ajili ya wachezaji na benchi la ufundi.

Jezi maalumu kwa ajili ya wapenzi na mashabiki zitapatikana katika sehemu mbalimbali huku bei ikiwa ni shilingi elfu 30 na zile wanazovaa wachezaji zitauzwa kwa shilingi laki moja na elfu ishirini.

Pia timu hiyo itaweka jiwe la msingi siku ya jumatatu ijayo katika uwanja wa mazoezi unaojengwa eneo la bunju jijini Dar es salaam ambapo uwanja huo umefikia hatua ya kuwekwa nyasi bandia ikielekea katika kilele cha wiki ya Simba sc.

Kampuni hiyo itakuwa inatoa shilingi milioni 300 kila mwaka ambazo milioni 200 zitakuwa ni vifaa na jezi wakati milioni 100 zitaingia katika klabuni.

Leo saa 6 usiku klabu ya Simba itazindua rasmi jezi zake kupitia mitandao yake ya kijamii ya Facebook, Tweeter na Instagram ambazo zitakuwa za aina tatu Nyekundu kwa mechi za nyumbani, Nyeupe za ugenini na Kijivu ambazo ni neutral kwa mujibu wa maelekezo ya Shirikisho la soka Afrika (CAF). Jezi hizo za Simba zitaanza kuuzwa kesho kwa bei ya shilingi 30,000 ambapo kwa hapa Dar es Salaam zitapatikana kwenye maduka ya Uhlsports Posta, Uhlsports Kariakoo, Uhlsports Sinza, Shaffih Dauda Sinza na Club ya Sinza.

Majuma kadhaa yaliyopita klabu ya Simba iliingia mkataba na kampuni ya A-one wazalishaji kinywaji cha Mo Extra mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi milioni 250.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka