Connect with us

Soka

Simba bingwa kombe la FA 2020/2021

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho baada ya kumfunga mtani wake wam jadi Yanga soka kwa goli 1-0.

Simba ilijipatia bao lake pekee la ushindi katika dakika ya 82 kupitia kwa Tadeo Lwanga aliyeunganisha krosi ya kona kutoka kwa Luis Miquissone na kumshinda mlinda mlango wa Yanga Farouk Shikalo.Katika mchezo huo kiundo wa Yanga Mukoko Tonombe alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko John Bocco.

Huu ni ubingwa wa pili mfululizo wa Simba katika michuano baada ya ule wa mwaka jana wakiifunga Namungo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka